Ticker

6/recent/ticker-posts

MADA 01-UUNDAJI WA MANENO

 

MADA 01-UUNDAJI WA MANENO 

Uundaji wa maneno ni shughuli ya kuunganisha viambajengo (vipashio) mbalimbali ili kupata maneno tofauti yenye maana mbalimbali ambazo ni kamili. 

Kwa kuwa maendeleo ya jamii hubadilika, hukua na kuongezeka hivyo hivyo lugha nayo hukua na kubadilika kwa lengo la kukidhi haja ya mawasiliano. 

Ili msamiati uongezeke lazima maneno yaundwe kwa lengo la kuboresha mawasiliano kulingana na wakati uliopo. 

UMUHIMU WA UUNDAJI WA MANENO 

  1. Kupata msamiati wa kutosha katika lugha husika ili kukidhi mabadiliko yanayojitokeza. 

  2. Kukabiliana na suala la maendeleo ya sayansi na teknolojia katika ongezeko la maneno mapya. 

  3. Ubunifu wa maneno mbalimbali hutokana na njia mbalimbali kama vile uambishaji wa maneno, kubadili mpangilio wa herufi kutohoa maneno ya lugha nyingine, kuambatanisha maneno, kufananisha sauti, umbo, mlio. 

UUNDAJI WA MANENO KWA KUTUMIA MOFIMU

(a)  MOFIMU 

1. Maana 

Mfano; Baba, Mungu, Fikiri, bora 

Katika Kiswahili, mofimu inaangaliwa katika daraja la vipashio vya lugha. kipashio hiki hakiwezi kuvunjwavunjwa zaidi bila kupoteza maana. 

Mfano:  

1. Mtoto (Watoto) 

AINA ZA MOFIMU 

Kuna aina kuu mbili za mofimu 

  1. Mofimu huru (sahihi) 

  2. Mofimu tegemezi 

  1. MOFIMU HURU/ SAHIHI 

Ni mofimu inayoweza kusimama peke yake na kuweza kutumiwa katika tungo bila kuwa na kiambishi chochote. Mofimu huru zina hadhi ya neno na zinaweza kuwa aina yoyote ya neno kama vile: - 

  1. MOFIMU TEGEMEZI 

Ni mofimu zinazofungamana na mofimu nyingine na zinapotumika hutegemeana ili kueleza dhana iliyokusudiwa. Mofimu hizi zinapofungamana huunda neno. Mofimu zinazounda neno huweza kuwa mbili au zaidi kulingana na mchangamano wa dhana ulio katika neno linaloundwa 

Mfano

Mtoto    -   m- toto 

Watacheza   -  wa – ta – chez – a 

Anasoma  -  a – na – som –a 

Mkulima   -  m – ku – lim –a 

NAFSI 



Mfano:- 

Neno “analima” lina mofimu nne (4) ambazo hufungamana na kujenga neno “analima” kila moja ya mofimu hizi isimamapo peke yake haina maana yoyote isipokuwa ina maana kisarufi ambayo humuwezesha mwanaisimu kuchambua maana ya mofimu hiyo. 

            Analima - a – na- lim – a 

 A – kiambishi awali kipatanishi cha nafsi ya III umoja 

Na – kiambishi awali cha wakati uliopo 

Lim – mzizi wa neno 

A – kiambishi tamati 

Dhima kuu ya mofimu ni kuongeza msamiati. Msamiati huo unaweza kuongezeka kwa kuunda neno zima. Pia msamiati unaweza kuundwa kwa shina moja kwa kuweza kuunda na kutoa maneno yenye maana mbalimbali. 

Mfano:- 

Neno “cheza” linaweza kuwa : mchezaji, mchezo, wanachezea, tulicheza, uchezeshaji, alimchezesha n.k. 

Vilevile mofimu tegemezi zina dhima mbalimbali tofauti na uundaji wa msamiati. Baadhi ya dhima hizi ni kama vile, 

  1. kudokeza nafsi 

  2. kuonesha njeo (wakati) 

  3. kuonesha/ kudokeza urejeshi 

  4. kudokeza ukanushi 

  5. kudokeza kauli mbalimbali 

(b)  UUNDAJI WA MANENO KWA KUTUMIA UAMBISHAJI  

(i)   Maana 

-      Uambishaji ni kitendo cha kupachika kiambajengo (mofimu) cha neno kwenye mzizi wa neno ili kukamilisha muundo wa neno 

VIAMBISHI  

 

                            AU 

                            

                              AU -  Viambishi ni mofimu zinazowekwa kwenye mzizi wa neno na kukamilisha muundo wa neno. 

Kwa mfano neno:  ANAYEJIPIKIA 

Viambishi awali (mwanzoni) vyake ni A – NA- YE – JI 

Viambishi tamati ni –I – A – na mzizi wa neno hilo ni – PIK- 

AINA ZA VIAMBISHI 

(a) Viambishi awali  

-   Hivi ni viambishi vinavyowekwa kabla ya mzizi wa neno navyo ni vitano 

(ii)  Viambishi ngeli Mfano: 

M – tu  =   wa – tu 

M – ti   =  mi – ti 

M – zuri  =  wa – zuri 

M – safi  =  wa – safi 

(iii) Kipatanishi (kiambishi awali cha nafsi) 

Hivi hujitokeza katika vitenzi na wakati fulani huitwa viambishi awali vya nafsi 

Mfano: -               Umoja                                     Wingi 

                        Ni – nalima                         tu – nalima (nafsi 1) 

                        U – nalima                          m – nalima (nafsi 2) 

                        A – nalima                          wa – nalima ( nafsi 3) 

(iv) viambishi awali vya wakati (njeo) 

Hivi huonesha wakati tendo limefanyika katika kitenzi 

Mfano: analima 

A – na- lima  (wakati uliopo) 

A – li – lima   (wakati uliopita) 

A – ta – lima  (wakati ujao) 

(v)  Viambishi awali vya hali 

Hivi huonesha hali mbalimbali katika kitenzi 

Mfano: - 

Hu – lima   (hali ya mazoea) 

A – me – lima   (hali timilifu) 

A-   nge – lima  ( hali ya masharti) 

(vi)  viambishi awali vya rejeshi vya mtendaji wa jambo au tendo (kiima) 

Hivi hutaja mtenda wa jambo 

Ni – na- ji – kata 

A – na – ye – sema 

U – li – o – enea 

(vii) Viambishi awali rejeshi vya mtendwa 

Hivi hutaja mtendwa wa jambo 

Mfano: - Tuli – u – panda 

Nina – i – soma 

Ana – m – piga 

Wana – ni – soma   

(viii) Viambishi awali vikanushi na yakinifu 

Hivi huwekwa katika kitenzi ili kukamilisha hali ya kukanusha, viambishi vya kukanusha katika lugha ya Kiswahili ni ha – hu – na – si 

Mfano: - 

U – naimba            hu – imbi 

Ni – nacheza             si – chezi 

A – naimba               ha- imbi 

(b)  Viambishi kati  

Ni viambishi vinavyopachikwa ndani ya mzizi wa neno na hivyo kuukuta katika sehemu mbili. 

Viambishi kati havitokei katika Kiswahili lakini vipo katika sehemu nyingine, mfano kiebrania. 

(c)  Viambishi tamati  

Hivi ni viambishi vinavyoambishwa baada ya mzizi wa neno navyo ni vya aina mbili. 

(i)    Viambishi tamati maana 

Hivi hutokea baada ya mzizi wa kitenzi bila kubadilisha umbo la mzizi wenyewe. Viambishi tamati maana hutaja maana au dhana. 

Mfano: - 

Lim –a 

Lim – wa 

Chez – a 

Chez – wa 

(ii)  Viambishi tamati vijenzi 

Hivi ni viambishi vinavyoandikwa baada ya mzizi wa kitenzi viambishi tamati vijenzi navyo hutokea mara baada ya mzizi wa kitenzi na vina kazi kuu nne. 

  1. Kuleta maana ya ziada ya kule kwenye maana ya asili iliyobebwa na mzizi wa kitenzi. 

Mfano: - 

Lima – limia- limika – limisha – limiwa 

Tendo – tendea – tendeka – tendesha – tendewa 

  1. Kujenga mzizi mpya wa kitenzi ambao utabebeshwa maana ya asili ya kitenzi na maana ya ziada. Mzizi huu mpya huitwa “mzizi wa mnyambuliko” 

Mfano: - 

  

(d)  Huweza kubadili neno toka aina moja na kuingia aina nyingine 

Mfano: - 

Omba – ombeana – ombaji – ombeka – ombi – ombeaji           

  T              T          N            T           N          T 

(e)  Kuweza kuzalisha kauli mbalimbali za tendo kama ifuatavyo;-                                

 

Kauli ya kutenda;-        Chez – a                                     Chek – a 

                                   Imb – a 

Kauli ya kutendwa;-      Chez – wa 

                                   Chek – wa 

                                   Imb – wa 

Kauli ya kutendeka;-      Chez – ek – a 

                                   Chek – ek – a 

                                   Imb – ik – a 

Kauli ya kutendewa;-      Chez – ew –a 

                                  Chek – ew – a                                    Imb – iw – a 

Kauli ya kutendea           Chez –e –a 

                                    Chek – e – a 

                                    Imb –i –a 

Kauli ya kutendeana       Cheze – an – a 

                                   Cheke – an – a 

                                   Imbi – an – a 

Kauli ya kutendesha       Cheze – sh – a 

                                   Cheke – sh – a 

                                   Imbi – sh – a 

(a)  MZIZI KIINI CHA KITENZI 

Mzizi au kiini ni ile sehemu ya neno inayobakia baada ya kuondolewa aina zote za viambishi yaani viambishi awali na tamati (mzizi ni sehemu isiyobadilika). 

Kuna aina mbili za mzizi 

(i)    Mzizi asilia 

Huu ni mzizi unaobakia baada ya kuondolewa viambishi tamati vijenzi. Mzizi huu mpya hubeba maana ya ziada ya hivyo viambishi maana kama vile: 

                       NENO                                                MZIZI ASILIA 

                          Lima                                                 lim- 

                         Lewa                                                 lew-                          Cheza                                               chez- 

                         Ona                                                   on- 

(ii) Mzizi mnyambuliko 

          Huu ni aina ya mzizi ambao hujengwa na mzizi asilia pamoja na viambishi tamati vijenzi. Mzizi huu mpya hubeba maana ya ziada ya hivyo viambishi. 

Kitenzi           Mzizi asilia               Mnyambuliko          Mzizi mnyambuliko 

Tema              tem                          Temana                      Teman 

Pata                Pat                            Patisha                      Patish 

Lia                   Li                              Lilika                          Lilik 

Kula                Kul                            Liwa                           Liw 

Soma              Som                          Somana                      Soman 

(b)  SHINA LA KITENZI 

Shina la kitenzi ni mzizi wowote (yaani mzizi asilia au mzizi wa mnyambuliko) uliofunguliwa irabu -a- isiyo na maana maalum ya sarufi. 

Mzizi                         shina 

Lim + a                      lima 

Chez + a                   cheza 

Fik +a                       fika 

Liw +a                       liwa 

Vitenzi vyenye asili ya kigeni ambao huishia na irabu e, i, u katika mzizi asilia yao. 

Mfano: - 

Vitenzi hivyo, mzizi asilia na shina huwa kitu kimoja 

Mzizi = shina + a 

Shina  = mzizi + a 

KUBAINISHA MOFIMU AU VIAMBISHI 

Kubainisha mofimu (viambishi) ni kitendo cha kutenga neno katika mofimu au viambishi vinavyolijenga. 

HATUA MUHIMU KATIKA KUBAINISHA MOFIMU 

Hatua zifuatazo ni muhimu katika kubainisha mofimu nazo ni: - 

  1. Kutambua aina ya neno ( neno huru au changamano) huundwa na mofimu tegemezi. Neno huru halivunjwivunjwi lakini neno changamano linavunjwavunjwa na kubainisha mofimu zake. Mfano wa neno huru  =  dada, kaka, mama. 

Mfano wa neno changamano  =   a – na – on – a 

                                           =   anaona 

  1. Kutenga (kuvunjavunja) mofimu au viambishi vinavyounda neno hilo yaani tambua viambishi awali, mzizi, kiini na viambishi tamati. Viambishi na mzizi hupatikana katika neno changamano 

Mfano: - 

Bainisha mofimu katika maneno yafuatayo na eleza kazi za kila mofimu. 

  1. Anasoma  -     a – na- som – a 

                         1     2     3     4 

  1. Kiambishi awali kipatanishi nafsi III umoja 

  2. Kiambishi awali cha wakati uliopo 

  3. Mzizi wa kitenzi 

  4. Kiambishi tamati 

  1. Dunia  -    hili ni neno huru ambalo huundwa na mofimu hizi hazivunjwivunjwi 

  2. Waliompiga  -  wa – li- o – m – pig – a 

                             1       2   3   4     5     6 

  1. Kiambishi awali kipatanishi nafsi ya tatu wingi 

  2. Kiambishi awali cha wakati uliopita 

  3. Kiambishi awali rejeshi cha watenda 

  4. Kiambishi awali rejeshi cha watendwa 

  5. Mzizi wa kitenzi 

  6. Kiambishi tamati 

DHIMA YA MOFIMU/ VIAMBISHI 

1. Kuonesha nafsi katika kitenzi 

Mfano: - 

Ni – nasoma= Tu – nasoma  - I 

U – nasoma   =  m – nasoma   - II 

A – nasoma   =  wa – nasoma- III 

2. Kuonesha njeo katika vitenzi 

Mfano: - 

A – na – cheza   -   wakati uliopo 

A – li – cheza   -    wakati uliopita 

A – ta – cheza -    wakati ujao 

  1. Kuonesha umoja na wingi katika nomino na viambishi 

Mfano: - M – toto =  wa – toto 

Ki – su  =   vi -su 

  1. Kuonesha hali mbalimbali za kitenzi 

Mfano: - hali ya masharti 

A – ki – ja 

A – nge – ku – ja 

Mfano: -   ni – nalima   -   si – limi 

  1. – nacheza  -   ha – chezi 

               U – naimba   -  hu – imbi 

  1. Kuonesha urejeshi wa mtenda au mtendwa katika kitenzi 

Mfano: -   A – na – ye – lima    -   Mtenda 

  1. – na – u – penda   -   mtendwa 

  1. Kuonesha kauli mbalimbali za vitenzi 

Kauli ya kutenda      - a – na – pik - a 

Kauli ya kutendea    - a – na -pik -i – a 

Kauli ya kutendewa-   a – na – pik – iw – a 

Kauli ya kutendeana   - wa – na – pik – ian – a 

Kauli ya kutendesha    -  a – na – pik - ish – a 

Kauli ya kutendwa   -   a – na – pik – w – a 

TOFAUTI YA MOFIMU NA SILABI 

 

NA 

 

MOFIMU 

 

SILABI 

  

  

Mofimu ni kipashio cha kiima chenye maana kisarufi na kileksia kamusi 

  

Ni sehemu ya neno ambayo huweza kutamkwa mara moja na kwa pamoja kama fungu la sauti 

  2

  

Kila mofimu ina kazi maalum kisarufi 

  


(mfano) analima 

A – na – lim – a 

Si kila silabi ina kazi maalumu mfano silabi ''bali" ikisimama peke yake haiwakilishi maana yoyote kisarufi 

  

  3

  

Katika mofimu kuna viambishi awali na tamati 

  

Katika silabi hakuna viambishi hivyo 

  

  4

  

Katika mofimu kuna mizizi, shina la neno 

  

Katika silabi hakuna mzizi wala shina. 

  5

  

Mofimu huru hazivunjwivunjwi, hubaki zilivyo mfano; neno baba lina mofimu huru moja 

  

Silabi huvunjavunja hata mofimu huru mfano; baba – ba + ba = silabi mbili 

  6

  

Mofimu hazivunjivunji mzizi wa neno mfano; 

Lima mzizi lim 

  

Silabi huvunjavunja mzizi wa neno mfano; “analima” lina silabi nne 

A -   na - li - ma 

1     2       3     4 

  7

  

Mara nyingi katika neno kuna idadi ndogo ya mofimu. Mfano; “mama” lina mofimu moja, anacheza lina mofimu nne 

  

Mara nyingi katika neno kuna idadi nyingi za silabi. Mfano; 

Mama – lina silabi mbili 

Anacheza – lina silabi nne 

  

(c)  UUNDAJI WA MANENO KWA KUTUMIA MNYAMBULIKO 

Unyambulishaji unatokana na neno “nyambua” ikiwa na maana refusha au vuta kitu. 

         Mnyambuliko ni kitendo cha uvutaji au urefushaji kipashio / vipashio katika mzizi wa neno. Aidha mnyambuliko unahusu upachikaji wa mofimu zinazofuata mzizi wa neno. Mofimu hizi huitwa mofimu fuatishi (viambishi tamati) 

Mfano:- 

Soma -  Som – e – a 

             Som – ek –a 

             Som – esh – a 

             Som – w – a 

             Som – ean – a 

              Som – o 

Vitenzi  

Vitenzi vyote vya Kiswahili isipokuwa kitenzi kishirikishi “ni” vinaweza kunyambulika. 

Mfano: - 

Piga – pigia, pigana, pigisha, pigwa, pigiana, cheza, chezea, chezeana, chezeshwa, chezwa. 

Baadhi ya majina ya ujumla hupokea viambishi tamati na mengine hupokea viambishi tamati vijenzi. 

Mfano: - 

Nyumba  -   nyumbani 

Bustani   -   bustanini 

Hewa     -   hewani 

Maji       -   majini 

Viwakilishi 

Hivi huchukua viambishi tamati maana 

Mfano: - 

  1. Viwakilishi vya nafsi kama vile 

Mimi     -  miye 

Wewe   -  weye 

Sisi       - siye 

Ninyi    -  niye    

  1. Viwakilishi virejeshi vya amba. 

Vivumishi 

Hivi huchukua viambishi tamati vijenzi 

Mfano: -         

Safi     -   safisha, safishwa, safishia, safishika 

Fupi    -  fupika, fupisha, fupishika, fupishwa 

Refu    -   refusha, refushwa, refushika 

Viunganishi 

Hesabu ndogo ya viunganishi huchukua viambishi tamati vitenzi. 

Mfano : - Labda, labdatisha, labdilika, labdishwa. 

DHIMA YA MNYAMBULIKO 

  1. Mnyambuliko wa maneno hukuza msamiati wa lugha husika. 

  2. Mnyambuliko wa maneno hupanua maana ya maneno. 

  3. Mnyambuliko wa maneno huzalisha kauli mbalimbali za vitenzi kutenda, kutendwa, kutendea, kutendeka, kutendana, kutendeana kutendesha, kutendeshwa.   

 

Post a Comment

0 Comments