TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
HALMASHAURI YA WILAYA YA HAI
MTIHANI WA MAANDALIZI KIDATO CHA NNE
KISWAHII-2021 D A MUDA: SAA 3:00
Maelekezo:
Karatasi hii ina sehemu A,B na Czenye jumla ya maswali kumi na mbili (12)
Jibu maswali yote katika sehemu A na B na maswali matatu(3) kotoka katika sehemu C.
Zingatia maagizo ya kila sehemu ya kila swali.
Simu ya mkononi na vitu vyote visivyoruhusiwa havtakiwi katika chumba cha mntihani
Andika nanba yako ya mtihani katika kila ukarasa wa kujibia.
SEHEMU A (ALAMA 15)
1. Jibu maswali yote katika sehemu hii.
i. Ni aina ya wahusika ambao hawabadiliki na wamepewa majina ambayo humfanya msomaji aelewe tabia na matendo yao
wahusika wakuu
wahusika bapa sugu
wahusika duara
wahusika bapa vielelezo
wahusika shinda
ii. vishazi tegezi vimegawanyika katika aina kuu mbili
vishazi tegemezi viwakilishi na vielezi
vishazi tegemezi vivumishi na viunganishi
vishazi tegemezi vivumishi na vielezi
vishazi tegemezi vikuu na visaidizi
vishazi tegemezi nomino na vihusishi
iii. Anatoa ufafanuzi juu ya ubantu wa Kiswahili kwa kueleza wakazi wa mwambao waliojulikana kama "Wazanji" na watawala wao waliojulikana kama "Wakilimi
Ali- idris
Al masudi
Marco polo
Ibin Batuta
Fumo Lyongo
iv. Ni lahaja zinazopatikana Mombasa
kitumbatu, kingazija, kimvita na kingare
kizwani, kintang'ata, kimakunduchi na kimvita
kijomvu, kingare, chichifundi, na kimvita
kitumbatu, kingare, kimvita na chichifundi
kimvita, chichifundi, kingazija, na kijomvu
v. Mofimu KU iliyopigiwa mstari imebeba dhima gani katika kitenzi sikukumbuka.
ukanushi wakati uliopita
ukanushi nafsi ya kwanza umoja
kauli ya kutendeka
kiambishi kirejeshi
kudokea mtendwa
vi. sehemu ya mzizi asilia iliyoambikwa kiambishi "a" mwishoni
shina
mzizi huru
mofu
kauli
mofimu huru.
vii. Ni tamathali ya semi ambayo jina la mtu hutumiwa kwa watu wengine wenye tabia,mienendo, hulka au kazi sawa na mtu huyo.
Taniaba
Tabaini
Majazi
Tashtiti
Ritifaa
viii. Neno SHADARA limepatikana kwa kutumia njia gani ya uundaji wa maneno.
kutohoa
ufupishaji
miambatano
urudufishaji
kukopa
ix. Chama cha kukuza na kueneza Kiswahili "TAKILUKI" kilianzishwa mwaka
1964
1967
1979
1972
1965
x. Aina ya hadithi za ngano zenye wahusika wanyama tu hujulikana kama,
Hekaya
Hurafa
Istiara
soga
vigano
Swali | i | ii | iii | iv | v | vi | vii | viii | ix | x |
Jibu |