OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
HALMASHAURI YA MANISPAA YA MOSHI
KAMATI YA MITIHANI IDARA YA ELIMU SEKONDARI - 021 KISWAHILI
MTIHANI WA AWALI WA UPIMAJI KITAIFA KIDATO CHA PILI
Jumatano 25 Agosti 2021 Asubuhi Muda: 3:00
MAELEKEZO:
- Karatasi hii ina sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali kumi na mbili
- Jibu maswali yote katika sehemu A na B na maswali matatu kutoka sehemu C.
- Sehemu A ina alama kumi na tano(15), sehemu B alama arobaini(40) na sehemu C alama arobaini na tano(45).
- Zingatia maelekezo ya kila sehemu na kila swali
- Andika namba yako ya mtihani katika kila ukurasa wa karatasi ya kujibia
SEHEMU A (ALAMA 15)
Jibu maswali yote katika sehemu hii
- Chagua jibu sahihi katika vipengele (i-x) kisha andika herufi ya jibu sahihi.
(i) Katika mpangilio wa lugha ya Kiswahili, kipi ni kipashio kidogo kuliko vyote?
(a) Tungo
(b) Kirai
(c) Kishazi
(d) Sentensi
(e) Neno
(ii) Nyumba ile ni mali ya urithi, neno ile katika sentensi hii ni aina gani ya neno?
(a) Nomino
(b) Kielezi
(c) Kiwakilishi
(d) Kivumishi
(e) Kitenzi
(iii) Mashairi ya majibizano baina ya watu wawili au zaidi ni?
(a) Nyimbo
(b) Ngonjera
(c) Tenzi
(d) Semi
(iv) Barua rasmi mara nyingi zinakuwa na anuani ngapi?
(a) 1
(b) 2
(c) Hakuna jibu
(d) 3
(e) B na C ni sahihi
(v) Mzizi wa neno anakula ni?
(a) Kul
(b) Kula
(c) Ul
(d) L
(e) Ku
(vi) Majibizano baina ya watu wawili au zaidi wanapozungumza ni?
(a) Riwaya
(b) Dayolojia
(c) Mahubiri
(d) Hotuba
(e) Risala
(vii) Katika lugha ya Kiswahili kuna aina ngapi za vielezi?
(a) Moja
(b) Tatu
(c) Vinne
(d) Zaidi ya nne
(e) Hakuna jibu sahihi
(viii) Katika sababu zifuatazo ni ipi si sahihi kuhusu matumizi ya kamusi?
(a) Kujifunza lugha ya kigeni
(b) Kujua tahajia za maneno
(c) Kusanifisha maneno mapya
(d) Kubaini kategoria ya maneno
(e) Kujua maana ya maneno
(ix) Tarihi ni?
(a) Aina ya semi
(b) Aina ya hadithi
(c) Aina ya sanaa ya maonyesho
(d) Aina ya riwaya
(e) Aina ya tamthilia
(x) Vipera vya ushairi wa fasihi simulizi ni?
(a) Methali, semi, mashairi na tenzi
(b) Ngonjera, tenzi, nyimbo, na mashairi
(c) Vigano, nyimbo, ngonjera, nahau na siga
(d) Taarabu, mashairi na majigambo
(e) Ushairi, mashairi, soga na methali
i. | ii. | iii. | iv. | v. | vi. | vii. | viii. | ix. | x. |
---|