JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA SINGIDA MUNICIPAL COUNCIL 021 KISWAHILI
Time: 2:30 Hours JULAI 2023
MAELEKEZO:
Karatasi hii ina sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali kumi (10)
Jibu maswali yote
Majibu yote yaandikwe kwenye nafasi ulizopewa
Majibu yote yaandikwe kwa kalamu ya wino wa bluu au mweusi
Vifaa vyote vya mawasiliano haviruhusiwi katika chumba cha mtihani.
SEHEMU A (ALAMA 15)
1. Jibu maswali yote katika sehemu hii.
i) Sauti za lugha ambazo hutamkwa bila kuwepo kwa kizuizi chochote kwenye mkondo kwa hujulikana kama:-
sauti
Herufi
Irabu
Konsonanti
ii) Silabi zinazotokea katikati au mwishoni mwa kila mstari wa shairi huitwaโฆโฆโฆ.
Vina
Mizani
Sitiari
Vituo
iii) Kiimbo hufasiliwaje katika mazungumzo?
Kupanda na kushuka kwa mawimbi ya sauti
kuzungumza na kuongea kwa sauti
kuzungumza kwa kupandisha mawimbi ya sauti
kuzungumza kwa kushusha mawimbi ya sauti
iv) Dhana ipi kati ya hizi zifuatazo haina maana Zaidi ya moja?
Kaka amefua nguo
Nipe sahani ya kulia
Eva amenunua kanga
John amempigia mpira
v) Mkisi ameenda Dodoma. Neno Dodoma limetumika kama
Kihisishi
Nomino
Kiwakilishi
Kielezi
vi) Mawazo makuu ya mtunzi wa kazi ya fasihi humfikia mlengwa kwa njia ipi kati ya hizi zifuatazo.
Fani
Falsafa
Migogoro
Dhamira
vii) Ipi ni tofauti ya msingi kati ya mashairi na ngonjera?
Mpangilio wa vina na mizani
Idadi ya mizani na mishororo
Majibizano baina ya watu wawili au Zaidi
Mpangilio wa silabi na lugha ya mkato.
viii) Bosi samahani kuna barua yako hapa โMtindo huu wa mazungumzo unatumika wapiโ?
Ofisini
Kiwandani
Shambani
Kanisani
ix) Sababu zifuatazo husababisha kutokea kwa utata katika tungo isipokuwa
Neno kuwa na maana Zaidi ya moja
Kuzingatia taratibu za uandishi
Kutumia maneno yenye maana ya picha
Kutotamka neno ulilokusudia kwa usahihi
x) Seti ipi ni sahihi kuhusu vipengele vya fani katika fasihi simulizi?
Dhamira, migogoro, mtindo na mafunzo
Ujumbe, matumizi ya lugha, wahusika, mtindo na muundo
Wahusika, matumizi ya lugha, muundo, mtindo na mandhari
Migogoro, Ujumbe,wahusika, mafunzo na mtindo