ST. MARYโS MBEYA SECONDARY SCHOOL
MTIHANI WA MWISHO WA MUHULA WA KWANZA KIDATO CHA TATU JULAI 2022 MSIMBO: 021 KISWAHILI
Muda: Saa 2:30
MAELEKEZO:
Karatasi hii ina sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali kumi na mbili (12).
Jibu maswali yote katika sehemu A na B na maswali matatu (3) kutoka sehemu C.
Sehemu A ina alama kumi na tano (15), sehemu B alama arobaini (40) na sehemu C ina alama arobaini na tano (45).
SEHEMU A (ALAMA 15)
Jibu maswali yote katika sehemu hii.
1. Chagua herufi ya jibu sahihi katika vipengele (i) hadi (x), kisha andika herufi ya
jibu hilo kwenye kijitabu chako cha kujibia.
i.Neno โChawaโ lenye maana ya mfuasi au kibaraka wa mtu fulani linaweza kuingizwa kwenye kundi gani la misimu kati ya haya?;
Misimu ya pekee
Misimu ya kihuni
Misimu bandia
Misimu ya kitarafa
Misimu zagao
ii. โMzee Mitomingi amelewa pombeโ. Je, neno Mitomingi katika tungo hii limetumika kama aina gani ya kivumishi?
Kivumishi cha pekee
Kivumishi cha jina kwa jina
Kivumishi cha sifa
Kivumishi cha namna
Kivumishi cha idadi
iii.Mwalimu wa Kiswahili alisikika akifundisha wanafunzi namna ya kufuatisha maneno katika sentensi ili kuleta maana sahihi.Kwa kuzingatia sarufi ya Kiswahili, je,mwalimu alikuwa anafundisha tawi lipi la sarufi kati ya haya?:
Sarufi Matamshi
Sarufi Muundo
Sarufi Maana
Sarufi Maumbo
Sarufi Mofolojia
iv. Mzee Mwakipesile ana watoto watano, wanne kati ya hao wamebatizwa majina kutoka nomino za pekee na mmoja amebatizwa jina kutoka nomino za dhahania.Je, unafikiri mtoto wa mzee Mwakipesile ambaye ana jina kutoka nomino za dhahania atakuwa nani kati ya hawa?;
Januari
Faraja
John
Amosi
Masanja
v.Mkuu wa shule wakati anawashauri wanafunzi waliofanya vibaya mtihani alisema kazeni kamba .Je,mkuu wa shule alitumia kipera gani cha semi kuwasihi wanafunzi wake kuongeza bidii?
Nahau
Methali
Kitendawili
Mizungu
Msemo
vi. Mwajuma ni mvuvi mahiri katika ziwa Nyasa na hupenda kuimba nyimbo za kujiliwaza awapo katika shughuli zake za uvuvi.Je, nyimbo zinazoimbwa katika muktadha huu kifasihi huitwaje?
Kimai
Tendi
Wawe
Kongozi
Nyiso
vii. Wakati wa sherehe za Mei mosi mwaka huu,wafanyakazi walishuhudia ushairi wa malumbano kuhusu ipi ni kazi muhimu kati ya udaktari na ualimu na mwishowe watambaji walikubaliana kuwa kazi zote ni muhimu kwa jamii. Je, unafikiri wafanyakazi walikuwa wanashuhudia kipera gani kati ya hivi?
Maghani
Majigambo
Ngonjera
Tenzi
Tendi
viii. โIli kamusi iweze kutumika katika utafiti wa chimbuko la lugha ni lazima iwe inafafanua asili za manenoโ Je,ni msamiati gani katika kamusi hutumika kumaanisha asili ya neno?
Kisawe
Vitawe
Etimolojia
Homonimu
Kibadala
ix. Rukia alipoulizwa swali lililomtaka abainishe dhima tano za viambishi awali,alitoa hoja nne zilizo sahihi na hoja moja isiyosahihi.Ibaini hoja moja ya Rukia ambayo haikuwa sahihi miongoni mwa hizi;
Kudokeza kauli mbalimbali
Kudokeza njeo
Kudokeza nafsi
Kudokeza ukanushi
Kudokeza urejeshi
x. Mhusika Sekai katika riwaya ya Takadini alikataa kuolewa na Manyamombe Kwa sababuโฆโฆโฆโฆโฆโฆโฆโฆโฆโฆโฆโฆ;
Sekai hakumpenda Manyamombe
Manyamombe alikuwa mzee mno
Hakutaka kutenganishwa na Takadini
Manyamombe alikuwa masikini
Manyamombe alikuwa na wake wengi