MARKAZ ISLAMIC SEMINARY
JARIBIO LA MUHULA WA KWANZA KIDATO CHA TATU
KISWAHILI-021
Aprili, 2024-Saa: 3:00
MAELEKEZO
Karatasi hii ina sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali kumi na moja(11).
Jibu maswali yote katika sehemu A na Bna maswali mawili (2) Kutoka sehemu C.
Sehemu A ina alama kumi na sita (16), sehemu B alama hamsini nne(54) na sehemu C ina alama thelathini (30).
Zingatia maelekezo ya kila sehemu na kila swali.
Simu za mikononi na vitu vyote visivyoruhusiwa havitakiwi katika chumba cha mtihani.
Andika Jina lako kamili katika kila ukurasa wa kijitabu chako cha kujibia
SEHEMU A (Alama 16)
Jibu maswali yote katika sehemu hii
Katika kauli zifuatazo kauli ipi ina sifa tofauti na nyingine?
Haraka haraka haina Baraka
Aibu ya maiti aijuae mwoshwa
Asiyefunzwa na mamaye hufunzwa na ulimwengu
Amevaa miwani
Mchelea mwana kulia yeye
Sehemu ya lugha inavyoshughulikia maumbo katika sentensi
Sarufi sintaksia
Sarufi fonolojia
Sarufi semantiki
Sarufi mofolojia
Sarufi Sentensi
Mwalimu alipoingia darasani aliuliza “Nyote hamjafanya kazi yangu!. Kutokana na kauli aliyotoa mwalimu katika uzungumzaji mwalimu ametumia
Kiimbo cha kuuliza
Kiimbo cha mshangao
Kiimbo cha masharti
Kiimbo cha maelezo
Kiimbo cha mshtuko
“Kiatu kimepotea”. Sentensi hii inaweza kuwekwa katika kundi la ngeli ya ngapi
Tatu
Nne
Tano
Sita
Saba
Chagizo katika uchanganuzi wa sentensi hutumika katika mkabala wa
Kimapokeo
Kimuundo
Kisiasa
Kiupatanishi
Kisintaksia
Uchanganuzi wa sentensi katika mkabala wa kimuundo hujikita katika
Kiima na kiarifu
Kirai nomino na kirai kivumishi
Kirai nomino na kirai kitenzi
Kirai nomino na kishazi tegemezi
Kirai kitenzi na kishazi tegemezi
Nyuzi ulizoshonea zimekwisha. Viambishi vya O rejeshi katika sentensi ni
U-Z0 katika ngeli ya tano
O-ZO katika ngeli ya sita
YO-ZO katika ngeli ya sita
YO-ZO katika ngeli ya tano
YO-ZO katika ngeli ya nne
Zakia ni mwimbaji wa mashairi kila akiimba katika mshororo wa mwisho wa beti zake hufanana katika kila ubeti. Je tunaweza kuupa jina gani kati ya haya kishairi
Kituo bahari
Mshororo uradidi
Mshororo takriri
Kituo bahari
Kituo
Katika utumizi wa kazi za fasihi kuna jambo moja linalodhihirisha upekee wa mtunzi. Ni jambo gani hilo?
Muundo wa kazi husika
Mtindo wa kazi husika
Wahusika wakazi husika
Jina la mtunzi wa kazi husika
Jina la kazi husika
Zakia na Sumaiyyah walikubaliana kuwa “ Watamfulia mwalimu wao”. Je wazo hilo la Zakia na Sumaiya lipo katika kauli ipi katika ya hizi.
Kutendea
Kutendeana
Kutendewa
Kutendwa
Kutendeka
2. Oanisha dhana za kifungu A ili kurandana na dhana iliyopo kifungu B
-
KIFUNGU A
KIFUNGU B
Shamirisho
Chagizo
Ambatani
Changamani
Prediketa
Sahili
Ni sehemu ya sentensi inayokaliwa na kitenzi
Ni aina ya sentensi iliyojengwa kwa sentensi mbili au zaidi kwa kutumia kiunganishi
Ni aina ya sentensi inayokaliwa na vielezi ……
Ni aina ya sentensi inayoundwa na kishazi huru kimoja
Ni sehemu ya kielezi inayopatikana upande wa kiarifu
Ni sehemu ya sentensi inayokaliwa na nomino dhahania
Ni nomino inayopatikana upande wa kiarifu
Ni aina ya sentensi inayoundwa kishazi tegemezi kimoja au zaidi
Ni aina ya sentensi yenye muundo wa kirai na kiarifu
SEHEMU B (Alama 54)
3. Mwandishi huweza kumfinyanga mhusika kwa namna atakavyo. Thibitisha ukweli huu namna mwandishi wa riwaya ya Watoto wa Mama Ntilie alivyomfinyanga mhusika mwanaume. Kwa hoja Sita madhubuti
4.
Sentensi hutungwa kwa kufuata Viambajengo maalumu ambavyo huweza kuleta maana kamili katika sentensi hiyo. Thibitisha usemi huu kwa kutunga sentensi kutokana na Vipashio vifuatavyo
N + Ts + Ts + T
W + V + T + E
N + t + N + V
H + T
Kamusi ni kitabu chenye orodha ya maneno yanayopangwa kialfabeti na kutoa taarifa za lugha husika. Kutokana na kamusi zilizopo hapo chini eleza kundi la kamusi husika
Baba (n) ni mzazi wa kiume
Mama (n) ni mzazi wa kike, A female parent
Baba (n) ni mzazi wa kiume, A male parent- mmale yamtzalile mwana.
Sentensi huweza kuchanganuliwa kwa kutumia njia na mkabala maalum. Changanua sentensi ifuatayo kwa njia ya jedwali kwa mkabala wa kimuundo
“Mbuzi aliyenunuliwa jana amechinjwa leo asubuhi”
Kwa mifano madhubuti onesha muundo wa kirai nomino. Hoja sita
Katika utanzu wa semi katika kipera cha methali huwa zipo zenye kurandana. Thibitisha ukweli huu katika methali zifuatazo kwa kuandika methali inayorandana katika semi zilizopo hapo chini
Mimi nyumba ya udongo sihimili kishindo
Miruzi mingi humpoteza mbwa
Uzuri wa mkakasi ndani kipande cha mti
Usipoziba ufa utajenga ukuta
Subira yavuta heri
Uvivu nyumba ya njaa
8.
Mke wa kwanza Maduo, huyu ninamtukuza
Ni mponda kwa ukoo, Asili yake Homboza
Ametuletea koo, Jinale ni maangaza Amuoe mke gani, kaka Chebi jamani?
Na sasa anae Jina, mzuri tena kijana
Kutwa wakiongozana, mithili mapacha wana
Hata enzi ya korona, mikono walishikana
Amuoe mke gani, Kaka chebi jamani
MASWALI:
Kichwa cha shairi kinachofaa
Elezea mtindo uliotumika katika uundaji shairi hili na namna alivyoichezea lugha katika matumizi yake
Eleza kwa kutaja migogoro iliyojitokeza na suluhisho la mgogoro huo
SEHEMU C (Alama 30)
Jibu maswali mawili kutoka sehemu hii. swali la tisa (9) ni la lazima
Waandishi huweza kutumia mandhari na kuibua dhamira katika kazi zao. Thibitisha kauli hii namna mwandishi wa riwaya ya watoto wa Mama Ntilie alivyoweza kutumia mandhari katika kuibua dhamira. Hoja sita madhubuti
Miviga katika jamii ina hasara na faida zake. Dhihirisha usemi huu kwa kuelezea hasara za miviga kwa jamii. Tumia hoja sita madhubuti
Methali huweza kuelimisha na kukosoa jamii. Thibitisha usemi huu kwa kutoa methali tatu zinazoelimisha na methali tatu zinazokosoa. Huku ukielezea mafunzo hayo na ukosoaji wake.