๐‘ท๐’“๐’†๐’Ž๐’Š๐’–๐’Ž ๐‘ฝ๐’†๐’“๐’”๐’Š๐’๐’|๐‘ญ๐’–๐’๐’ ๐‘ท๐’๐’”๐’•๐’” ๐‘ผ๐’๐’๐’๐’„๐’Œ ๐‘ต๐’๐’˜

๐ŸŒŠPAPER 11~Qns

 

MARKAZ ISLAMIC SEMINARY

JARIBIO LA MUHULA WA KWANZA KIDATO CHA TATU

015-ELIMU YA DINI YA KIISLAMU

April, 2024-Saa: 3:00

MAELEKEZO

  1. Mtihani huu una sehemnu A, B na C zenye jumla ya maswali kumi (11).

  2. Jibu maswali yote kutoka sehemu A na B na maswali mawili kutoka sehemu

  3. Andika Jina lako kamili katika kila ukurasa wa kijitabu cha kujibia.

  4. Simu za mkononi na vyote visivyohusika na mtihani HAVIRUHUSIWI katika chumba cha mtihani.

  5. Soma vizuri maelekezo ya kila swali kabla hujaanza kujibu.





SEHEMU A: (Alama 16)

Jibu maswali yote katika sehemu hii

1. Katika kipengele (i) – (x) chagua jibu sahihi kisha andika herufi yake katika kijitabu chako cha kujibia.

  1. Muislamu aliyeelimika anaweza kukitambua chanzo cha elimu kuwa _______

    1. Allah (SW)

    2. Akili na vipawa vya mwanadamu

    3. Sayansinna teknolojia

    4. Mitume wa Allah (SW)

    5. Uzoefu wa Milango ya fahamu

  1. Uislamu unamtambua muumini wa kweli ni Yule ambaye:-

      1. Aliyeamini nguzo sita za Imani

      2. Aliyetamka shahada zote mbili

      3. Ni Yule aliyethibitisha imani yake kwa matendo

      4. Ni Yule mwenye yakini juu ya uwepo wa jambo

      5. Ni Yule anayeamini uwepo wa mwenyezi Mungu

  1. Zifuatazo ni njia za kumtambua Allah (SW) isipokuwa:-

      1. Nafasi ya Fitrah

      2. Mafundisho ya Mitume

      3. Nafsi

      4. Mazingira

      5. Nafasi ya vipaji vya mwanadamu

  1. “Matuminzi ya dini ni kuidumaza jamii kwa kuibakisha kwenye fikra za ujima, kuingyonya na kuidhulumu jamii” Hii ni:-

      1. Fikra ya Krl Max kuhusu kazi ya Dini

      2. Nadharia ya Lenin Kuhusu kazi ya DIni

      3. Kazi za dini za kijahilia

      4. Kazi ya dini kwa matazamo wa makafiri

      5. Kazi ya dini kwa mtazamo wa mayahudi na wakristo.

  1. Mtazamo wa wasiokuwa waislamu kuhusiana na chanzo cha dunia na mwanadamu

      1. Vimetokea kuwepo kwa bahati Nasibu

      2. Sokwe ambaye alibadilika taratibu

      3. Udongo wa mfinyanzi unaonata

      4. Mlipuko wa tufe uliogawika vipande vipande

      5. Ni maada ambayo haina mwanzo wala mwisho



  1. Mtu aliye na elimu ya Fiq-hi anaelewa kuwa “Fiq-hi muamalat” inahusiana na:-

    1. Mambo ya ibada maalumu

    2. Mambo ya makosa ya jinai

    3. Mambo yanayohusiana na jamii

    4. Mambo yaliyo hiari kuyafanya

    5. Mambo yanayomuhusu maiti

  1. Kwa mujibu wa tareikh ya Kiislamu wakaazi wa Bara Arab tabia na mwenendo wao ulikuwa:- A. Uadilifu na Huruma

    1. Upole na kusaidiana

    2. Dhulma na Ihsan

    3. Mwenendo na tabia njema

    4. Ubabe na unyang’anyi

  1. Kima cha chini kabisa cha mali ambacho mtu akiwa nacho anastahiki kutoa zakatat A. Niqaab

    1. Nisaab

    2. Masaab

    3. Zakat

    4. Sadakaa

  1. Watoto wawili ambao walimuuzia Mtume (SAW) uwanja uliotumika kujenga msikiti wa Qubah mara tu Mtume (SAW) alipohamia madina

    1. Suhail na Sahil

    2. Is-haq na Ismael

    3. Khalid na Walid

    4. Kabiil na Habiil

    5. Ubayda na Abu Amamah.

  1. Waelimishe wasiojua ni upi Wahyi wa kwanza alioshushiwa Mtume?

    1. Surat – Mudathir (74:1 - 7)

    2. Surat – Muzammil (73:1 - 10)

    3. Surat – Fat-ha (1:1-7)

    4. Surat Alaq (96:1-5)

    5. Surat – Baqara (2:1-10)

  1. Chagua kifungu cha maneno kutoka Orodha B kinachouwiana na kufungu cha maneno kutoka Orodha A. andika herufi ya jibu sahihi katika kila kipengele katika kijitabu chako cha kujibia.

ORODHA A

ORODHA B

  1. Nguzo ya funga

  2. Funga za kafara

  3. Yasiyobatilisha funga

  4. Sunnah za funga

  5. Yanayobatilisha funga

  6. Funga za sunnah

  1. Kunuia kula hali ya kuwa umefunga

  2. Masiku meupe

  3. Kufunga siku ya Arafa

  4. Kufunga miezi mitatu kwa aliyeua mtu kwa makusudi

  5. Kujizuilia na kila chenye kufunguza toka Alfajiri mpaka

Magharibi

  1. Kufunga siku tatu mfululizo kwa aliyevunja kiapo

  2. Kutokwa na manii

  3. Kuzidisha kusoma Qur-an

SEHEMU B: (ALAMA 54)

  1. a) Mwenye kumuamini Allah kimatendo huwa anakuwa na sifa gani?

    1. Orodhesha ishara tano za ujumla zinazothibitisha uwepo wa Allah.

    2. Taja faida mbili anazozipata mja anayemwamini Allah kikwelikweli

  1. a) Taja vitabu vinne vya Allah na Mitume waliopewa vitabu hivyo.

    1. Wewe kama kiongozi wa Kiislamu katika nchi inayofuata sharia za Allah, umeletewa watu waliofanya makosa ya unywaji pombe, wizi na uzinifu ilihali hawajapata ndoa. Utatoa hukumu gani kwa hawa kwa kuzingatia Qur’an na Sunnah?

  1. Makafiri wana hoja nyingi zisiyo na msingi sahihi juu ya uwepo wa Allah. Onesha hoja tatu tu kisha zidhaifishe kwa kutoa hoja madhubuti.

  1. Namna gani utamjuza mtu asiye amini uwepo wa Allah kwa kumuonesha alama zilizo mwilini mwake? Eleza hoja tatu.

  2. Wafahamishe wanafunzi wa kidato cha kwanza aina tatu za Tawhid kwa kuwaelezea namna zinavyopaswa kueleweka.

  1. Tumia njia ya jedwali kubainisha aina za Tawhid zinazoendana na matendo yafuatayo;

  1. Kuchinja

  2. Kutegemea

  3. Kuswali

  1. Kutukuza

  2. Kuomba mwongozo

  3. Kuomba uokovu



SEHEMU C (Alama 30)

Jibu maswali mawili (2) tu kutoka sehemu hii.

9.

      1. Mzee Mohammad ni mfanya biashara anayemiliki duka la vyakula halali, baada ya kupindukia mwaka akafanya mahesabu ya bidhaa zilizo dukani kwake akakuta bidhaa hizo zina thamani ya shilingi 3,000,000/=. Msaidie mzee huyu kutambua kama anastahiki kutoa Zakat au la, ikiwa anastahiki, msaidie kufanya mahesabu na kutambua ni kiasi gani kinastahiki kutolewa Zakat kwa mwaka huo?

      1. Bwana Ziad ni Mchimba madini maarufu katika mgodi wa King’ong’o, katika mwaka huu amefanikiwa kupata madini aina ya dhahabu kilogramu 1. Msaidie Bwana huyu kugawa Zakat ya mali yake hii baada ya kukidhi vigezo vyote vya utoaji wa Zakat.

      1. Bibi Zuwena ni Mkulima wa zabibu na nyanya mkoani Singida, katika mwaka huu amefanikiwa kuvuna zabibu pakacha 200 ambapo kila pakacha lilikuwa na ujazo wa kilo 5, na nyanya tenga 50 kila tenga lina ujazo wa 70. Pia anamiliki fedha taslimu shilingi 5,000,000/= zilizopindukia mwaka. Kwa kuzingatia vigezo vya utoaji wa Zakat, msaidie Bibi huyo kujua kinachostahiki kutolewa Zakat kwa ujumla wake.

    1. Hadithi za Mtume (Sallallahu Alayhi Wasallam) zimegawanywa kwa kuzingatia vigezo mbalimbali ikiwemo kigezo cha usahihi. Kwa kuzingatia kigezo hiki eleza aina nne za Hadithi hizo.

    1. Allah Mtukufu ameteremsha vitabu vingi vikiwemo Tawrat, Zabur, Injil na Qur’an, pamoja vitabu hivi vyote ni vyake lakini kuna tofauti sana baina yake. Chambua tofauti nne za msingi ziliozopo baina ya kitabu cha mwisho na hivyo vingine.

→Get a Copy←



Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.