MARKAZ ISLAMIC SEMINARY
JARIBIO LA MUHULA WA KWANZA KIDATO CHA TATU
015-ELIMU YA DINI YA KIISLAMU
April, 2024-Saa: 3:00
MAELEKEZO
Mtihani huu una sehemnu A, B na C zenye jumla ya maswali kumi (11).
Jibu maswali yote kutoka sehemu A na B na maswali mawili kutoka sehemu
Andika Jina lako kamili katika kila ukurasa wa kijitabu cha kujibia.
Simu za mkononi na vyote visivyohusika na mtihani HAVIRUHUSIWI katika chumba cha mtihani.
Soma vizuri maelekezo ya kila swali kabla hujaanza kujibu.
SEHEMU A: (Alama 16)
Jibu maswali yote katika sehemu hii
1. Katika kipengele (i) – (x) chagua jibu sahihi kisha andika herufi yake katika kijitabu chako cha kujibia.
Muislamu aliyeelimika anaweza kukitambua chanzo cha elimu kuwa _______
Allah (SW)
Akili na vipawa vya mwanadamu
Sayansinna teknolojia
Mitume wa Allah (SW)
Uzoefu wa Milango ya fahamu
Uislamu unamtambua muumini wa kweli ni Yule ambaye:-
Aliyeamini nguzo sita za Imani
Aliyetamka shahada zote mbili
Ni Yule aliyethibitisha imani yake kwa matendo
Ni Yule mwenye yakini juu ya uwepo wa jambo
Ni Yule anayeamini uwepo wa mwenyezi Mungu
Zifuatazo ni njia za kumtambua Allah (SW) isipokuwa:-
Nafasi ya Fitrah
Mafundisho ya Mitume
Nafsi
Mazingira
Nafasi ya vipaji vya mwanadamu
“Matuminzi ya dini ni kuidumaza jamii kwa kuibakisha kwenye fikra za ujima, kuingyonya na kuidhulumu jamii” Hii ni:-
Fikra ya Krl Max kuhusu kazi ya Dini
Nadharia ya Lenin Kuhusu kazi ya DIni
Kazi za dini za kijahilia
Kazi ya dini kwa matazamo wa makafiri
Kazi ya dini kwa mtazamo wa mayahudi na wakristo.
Mtazamo wa wasiokuwa waislamu kuhusiana na chanzo cha dunia na mwanadamu
Vimetokea kuwepo kwa bahati Nasibu
Sokwe ambaye alibadilika taratibu
Udongo wa mfinyanzi unaonata
Mlipuko wa tufe uliogawika vipande vipande
Ni maada ambayo haina mwanzo wala mwisho
Mtu aliye na elimu ya Fiq-hi anaelewa kuwa “Fiq-hi muamalat” inahusiana na:-
Mambo ya ibada maalumu
Mambo ya makosa ya jinai
Mambo yanayohusiana na jamii
Mambo yaliyo hiari kuyafanya
Mambo yanayomuhusu maiti
Kwa mujibu wa tareikh ya Kiislamu wakaazi wa Bara Arab tabia na mwenendo wao ulikuwa:- A. Uadilifu na Huruma
Upole na kusaidiana
Dhulma na Ihsan
Mwenendo na tabia njema
Ubabe na unyang’anyi
Kima cha chini kabisa cha mali ambacho mtu akiwa nacho anastahiki kutoa zakatat A. Niqaab
Nisaab
Masaab
Zakat
Sadakaa
Watoto wawili ambao walimuuzia Mtume (SAW) uwanja uliotumika kujenga msikiti wa Qubah mara tu Mtume (SAW) alipohamia madina
Suhail na Sahil
Is-haq na Ismael
Khalid na Walid
Kabiil na Habiil
Ubayda na Abu Amamah.
Waelimishe wasiojua ni upi Wahyi wa kwanza alioshushiwa Mtume?
Surat – Mudathir (74:1 - 7)
Surat – Muzammil (73:1 - 10)
Surat – Fat-ha (1:1-7)
Surat Alaq (96:1-5)
Surat – Baqara (2:1-10)
Chagua kifungu cha maneno kutoka Orodha B kinachouwiana na kufungu cha maneno kutoka Orodha A. andika herufi ya jibu sahihi katika kila kipengele katika kijitabu chako cha kujibia.
-
ORODHA A
ORODHA B
Nguzo ya funga
Funga za kafara
Yasiyobatilisha funga
Sunnah za funga
Yanayobatilisha funga
Funga za sunnah
Kunuia kula hali ya kuwa umefunga
Masiku meupe
Kufunga siku ya Arafa
Kufunga miezi mitatu kwa aliyeua mtu kwa makusudi
Kujizuilia na kila chenye kufunguza toka Alfajiri mpaka
Magharibi
Kufunga siku tatu mfululizo kwa aliyevunja kiapo
Kutokwa na manii
Kuzidisha kusoma Qur-an
SEHEMU B: (ALAMA 54)
a) Mwenye kumuamini Allah kimatendo huwa anakuwa na sifa gani?
Orodhesha ishara tano za ujumla zinazothibitisha uwepo wa Allah.
Taja faida mbili anazozipata mja anayemwamini Allah kikwelikweli
a) Taja vitabu vinne vya Allah na Mitume waliopewa vitabu hivyo.
Wewe kama kiongozi wa Kiislamu katika nchi inayofuata sharia za Allah, umeletewa watu waliofanya makosa ya unywaji pombe, wizi na uzinifu ilihali hawajapata ndoa. Utatoa hukumu gani kwa hawa kwa kuzingatia Qur’an na Sunnah?
Makafiri wana hoja nyingi zisiyo na msingi sahihi juu ya uwepo wa Allah. Onesha hoja tatu tu kisha zidhaifishe kwa kutoa hoja madhubuti.
Namna gani utamjuza mtu asiye amini uwepo wa Allah kwa kumuonesha alama zilizo mwilini mwake? Eleza hoja tatu.
Wafahamishe wanafunzi wa kidato cha kwanza aina tatu za Tawhid kwa kuwaelezea namna zinavyopaswa kueleweka.
Tumia njia ya jedwali kubainisha aina za Tawhid zinazoendana na matendo yafuatayo;
|
|
SEHEMU C (Alama 30)
Jibu maswali mawili (2) tu kutoka sehemu hii.
9.
Mzee Mohammad ni mfanya biashara anayemiliki duka la vyakula halali, baada ya kupindukia mwaka akafanya mahesabu ya bidhaa zilizo dukani kwake akakuta bidhaa hizo zina thamani ya shilingi 3,000,000/=. Msaidie mzee huyu kutambua kama anastahiki kutoa Zakat au la, ikiwa anastahiki, msaidie kufanya mahesabu na kutambua ni kiasi gani kinastahiki kutolewa Zakat kwa mwaka huo?
Bwana Ziad ni Mchimba madini maarufu katika mgodi wa King’ong’o, katika mwaka huu amefanikiwa kupata madini aina ya dhahabu kilogramu 1. Msaidie Bwana huyu kugawa Zakat ya mali yake hii baada ya kukidhi vigezo vyote vya utoaji wa Zakat.
Bibi Zuwena ni Mkulima wa zabibu na nyanya mkoani Singida, katika mwaka huu amefanikiwa kuvuna zabibu pakacha 200 ambapo kila pakacha lilikuwa na ujazo wa kilo 5, na nyanya tenga 50 kila tenga lina ujazo wa 70. Pia anamiliki fedha taslimu shilingi 5,000,000/= zilizopindukia mwaka. Kwa kuzingatia vigezo vya utoaji wa Zakat, msaidie Bibi huyo kujua kinachostahiki kutolewa Zakat kwa ujumla wake.
Hadithi za Mtume (Sallallahu Alayhi Wasallam) zimegawanywa kwa kuzingatia vigezo mbalimbali ikiwemo kigezo cha usahihi. Kwa kuzingatia kigezo hiki eleza aina nne za Hadithi hizo.
Allah Mtukufu ameteremsha vitabu vingi vikiwemo Tawrat, Zabur, Injil na Qur’an, pamoja vitabu hivi vyote ni vyake lakini kuna tofauti sana baina yake. Chambua tofauti nne za msingi ziliozopo baina ya kitabu cha mwisho na hivyo vingine.
→Get a Copy←