๐‘ท๐’“๐’†๐’Ž๐’Š๐’–๐’Ž ๐‘ฝ๐’†๐’“๐’”๐’Š๐’๐’|๐‘ญ๐’–๐’๐’ ๐‘ท๐’๐’”๐’•๐’” ๐‘ผ๐’๐’๐’๐’„๐’Œ ๐‘ต๐’๐’˜

๐ŸŒŠPAPER 47-Qns

 

MTIHANI WA MWISHO MWAKA

KIDATO CHA TATU

KISWAHILI   NOVEMBA 2023

Muda 2:30 

MAELEKEZO 

  1. Jibu maswali yote

  2. Mtihani huu una sehemu A. B na C (Jumla ya maswali 9)

  3. Simu za mkononi haziruhusiwi



SEHEMU A (16)

  1. Chagua jibu sahihi katika maswali yafuatayo

  1. Neno lipi kati ya haya ni mofimu huru

  1. Uji

  2. Uzuri

  3. Uchache

  4. Ufa

  5. Upweke

  1. Ni kauli inayotumia maneno ya kawaida lakini hutoa maana tofauti na iliyopo kwenye maneno yale.

  1. Mafumbo

  2. Nahau

  3. Misemo

  4. Semi

  5. Hadithi

  1. Utokeji wa misimu katika jamii hutegemea na

  1. Uchaguzi wa viongozi

  2. Mabadiliko ya Kijamii

  1. Shughuli itendekayo

  2. Utani uliopo miongoni mwa wanajamii

  3. Kutumia na kudumu kwa muda mrefu

  1. Nyenzo kuu za lugha ya Mazungumzo ni

  1. Usimuliaji

  2. Mdomo

  3. Maandishi

  4. Vitendo

  5. Ishara




  1. Kipi kipengele kinachohusu mjengeko wa kazi za fasihi?

  1. Muundo

  2. Wahusika

  3. Mtindo

  4. Mandhari

  5. Lugha

  1. Kikundi cha maneno kinachoonesha jambo lililotendwa na mtenda katika sentensi hujulikanaje?

  1. Kikundi kivumishi

  2. Kikundi kitenzi

  3. Nomino

  4. Chagizo

  5. Shamirisho

  1. ni kauli ipi iliyotumika katika uundaji wa neno “Nitamfitinisha”

  1. Kutendeana 

  2. Kutendesha

  3. Kutenda

  4. Kutendea

  5. Kutendewa

  1. Dhima Kuu ya Misima katika lugha ni ipi?

  1. Kuficha jambo kwa wasiohusika

  1. Kuongeza ukali wa maneno

  2. Kupatanisha maneno

  1. Kutambulisha aina za maneno

  2. Kuhimiza shughuli za maendeleo

  1. Ipi ni jozi sahihi ya vipera vya semi?

  1. Soga, nyimbo na nahau

  2. Methal mizungu na vitendawili

  3. Mafumbo, soga, maghani

  4. Misemo, mafumbo na vigano

  5. Mashairi mafumbo na mizungu

  1. Shule zetu zimeweka mikakati kabambe ya kutokomeza daraja la pili ili zibaki na daraja la kwanza pekee. Neno ‘ili’ katika tungo hii ni aina gani ya neno?

  1. Kiunganishi

  2. Kivumishi

  3. Kielezi

  4. KITENZI

  5. Kihusishi



Qns

i

ii

iii

iv

v

vi

vii

viii

ix

x

Ans













  1.  Oanisha maelezo yaliyo katika Orodha A na dhana husika katika Orodha B. Kisha andika herufi husika katika karatasi ya majibu.

 

ORODHA A

ORODHA B

  1. Mada, Uhusiano, Malengo na Muktadha

  2. Umeupiga mwingi

  3. Nani Ugali mbuzi choma

  4. Baba Juma amefariki

  5. Hupokea mabadiliko ya papo hapo

  6. Kutumia lugha kulingana na kaida za jamii

  1. Tungo tata

  2. Utumizi wa lugha

  3. Lugha ya mazungumzo

  4. Simo

  5. Rejesta

  6. Humsaidia mzungumzaji kuteua lugha kwa usahihi

  7. Sababu ya utata

  8. Lahaja

  9. Lugha ya maandishi

 


Orodha A

i

ii

iii

iv

v

Vi

Orodha B










SEHEMU B (ALAMA 54)

  1.        (a)Unaelewa nini dhana ya misimu

(b) Onesha vyanzo viwili vya Msimu

(c) Misimu huweza kuundwa kwa njia tofauti tofauti

  1. Demu

  2. Kumzimikia

  3. Disco

  4. Ferouz ni twiga

  5. Mataputapu

  1.        Batuli alitaka kuhifadhi methali na vitendawili kwa njia ya Kichwa tu kwa ajili ya kizazi kijacho. Lakini Kibutu alimkataza asifanye hivyo badala yake atumie njia nyingine

  1. Toa hoja nne (4) kama sababu ya katazo hilo

  2. Taja njia tano (5) sahihi ambazo unahisi kibuyu angemshawishi batuli atumie.

  1.        Eleza kinagaubaga tofauti zilizopo kati ya lugha ya mazungumzo na lugha ya maandishi kwa kuzingatia vipengele vifuatavyo.

  1. Uwasilishaji

  2. Uhifadhi

  3. Manadiliko

  1.        Lugha ina tabia ya kujiongeza msamiati wake kwa njia kadha wa kadha; kwa kuthibitisha dai hilo, tambulisha njia zilizotumika kuunda maneno yafuatayo.

  1. Kuku

  2. Mpangaji

  3. Kifaurongo

  1. TATAKI

  2. Fedha

  3. Msikwao

  1. Kitivo

  2. Pilipili

ix. Imla, mali, mila, lami 




  1.        Maendeleo ya Sayansi na Teknologia ni ndumi la kuwili kwa fasihi simulizi. Kwa hoja sita thibitisha ukweli wa kauli hii kwa kutoa hoja mbili.

8.  Soma kifungu habari kifuatacho kisha jibu maswali yanayofuata:

"Ndugu wazazi, kumbe safari yenu inahusu harusi ya Maria ?".Mkuu wa shule aliwauliza wazazi."Ndiyo," wazazi walijibu kwa Pamoja bila aibu."inategemewa kufugwa lini ."Mkuu aliendelea kuhoji. Harusi hii ilikuwa ifanyike wakati Maria anapofika kidato cha nne, Lakini Maria huyu ametufanyia uhuni na vituko visivyoelezeka. Nasi sasa tunachukiwa kijiji kizima na kudharauliwa na kila mtu.Hii imetuudhi sana, tumetungiwa nyimbo na kufanyiwa kila shutuma. Hatuna raha ;hivyo tumeonelea bora tuje kukuomba umfukuze shule ili kiburi kimwishie .Nasi tupo tayari kukulipa kiasi chochote cha fedha ukitimiza haja yetu hii,"Mzee Abdallah alieleza." Muda wote mkuu wa shule alikuwa akimtazama Mzee kwa chati sana .Kisha akauliza swali la kuchochea zaidi: Maria ana kiburi kumbe?"

Mama Maria hakutaka hilo limpite ,hima hima akatoa maelezo yake ."Mama wewe ,Maria usimuone hivi. Maria mwanangu hataki kufuata utamaduni wetu wa kuolewa. Maria ati achague mchumba mwenyewe, ati mahari haiyoni kama ni kitu cha msingi. Kiburi hicho kinatokana na elimu mliyompa.

Mtoto sasa ameharibika .Anafanya apendavyo elimu gani isiyojali adabu.wala utii?" Mama Maria alimaliza huku jasho na machozi yanamtoka".

Hapa mkuu wa shule aliona kwanza awaelimishe kabla hajawatolea kauli ya  mwisho.Alikwishatambua kwamba wazazi wa Maria walikuwa wameachwa nyuma na wakati .Kila upya wa mawazo waliuita kiburi.

Maswali

(i)Bainisha dhima nne (04) zilizotokana na habari uliyosoma.

Fupisha habari hiyo kwa maneno yasiyopungua 70 na kuzidi 80.

 

SEHEMU C: (ALAMA 30)

Jibu maswali mawili katika sehemu hii swali la 11 ni lazima 


ORODHA YA VITABU.

USHAIRI. 

RIWAYA. 

TAMTHILIYA

  • Orodha - Steve Reynolds(MA)

  • Ngoswe Penzi Kitovu Cha uzembe - E. Semzaba (ESC)

  • Kilio chetu - Medical Aid Foundation (TPH)

9.Fasihi ya Kiswahili imemuweka mwanamke katika hadhi tofauti tofauti. Thibitisha Usemi huu kwa kutumia hoja tatu kwa kila riwaya


 10.Lugha ni mhimili katika kazi yoyote ya fasihi. Watunzi hutumia lugha kiufundi ili kufikisha ujumbe kwa jamii husika. Kwa kutumia jazanda au taswira tatu kutoka katika diwani mbili ulizosoma na uonyeshe namna zinavyofikisha ujumbe kwa jamii.


11.   “Ukiona mtu mzima analia ujue kuna jambo au mambo hayapo sawa. Kauli hii inaweza kuwiana na waandishi wa riwaya Juu ya jamii inavyowazunguka, kwa kutoa hoja tatu kutoka kila riwaya katika riwaya mbili ulizosoma, jadili kwa nini wasanii hao hulia

The End|Get a Copy





Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.