MTIHANI WA MWISHO MWAKA
KIDATO CHA TATU
KISWAHILI NOVEMBA 2023
Muda 2:30
MAELEKEZO
Jibu maswali yote
Mtihani huu una sehemu A. B na C (Jumla ya maswali 9)
Simu za mkononi haziruhusiwi
SEHEMU A (16)
Chagua jibu sahihi katika maswali yafuatayo
Neno lipi kati ya haya ni mofimu huru
Uji
Uzuri
Uchache
Ufa
Upweke
Ni kauli inayotumia maneno ya kawaida lakini hutoa maana tofauti na iliyopo kwenye maneno yale.
Mafumbo
Misemo
Semi
Hadithi
Utokeji wa misimu katika jamii hutegemea na
Uchaguzi wa viongozi
Mabadiliko ya Kijamii
Shughuli itendekayo
Utani uliopo miongoni mwa wanajamii
Kutumia na kudumu kwa muda mrefu
Nyenzo kuu za lugha ya Mazungumzo ni
Usimuliaji
Mdomo
Maandishi
Vitendo
Ishara
Kipi kipengele kinachohusu mjengeko wa kazi za fasihi?
Muundo
Wahusika
Mtindo
Mandhari
Lugha
Kikundi cha maneno kinachoonesha jambo lililotendwa na mtenda katika sentensi hujulikanaje?
Kikundi kivumishi
Kikundi kitenzi
Nomino
Chagizo
Shamirisho
ni kauli ipi iliyotumika katika uundaji wa neno “Nitamfitinisha”
Kutendeana
Kutendesha
Kutenda
Kutendea
Kutendewa
Dhima Kuu ya Misima katika lugha ni ipi?
Kuficha jambo kwa wasiohusika
Kuongeza ukali wa maneno
Kupatanisha maneno
Kutambulisha aina za maneno
Kuhimiza shughuli za maendeleo
Ipi ni jozi sahihi ya vipera vya semi?
Soga, nyimbo na nahau
Methal mizungu na vitendawili
Mafumbo, soga, maghani
Misemo, mafumbo na vigano
Mashairi mafumbo na mizungu
Shule zetu zimeweka mikakati kabambe ya kutokomeza daraja la pili ili zibaki na daraja la kwanza pekee. Neno ‘ili’ katika tungo hii ni aina gani ya neno?
Kiunganishi
Kivumishi
Kielezi
KITENZI
Kihusishi
Qns |
i |
ii |
iii |
iv |
v |
vi |
vii |
viii |
ix |
x |
Ans |
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
Oanisha maelezo yaliyo katika Orodha A na dhana husika katika Orodha B. Kisha andika herufi husika katika karatasi ya majibu.
ORODHA A |
ORODHA B |
|
-
Orodha A
i
ii
iii
iv
v
Vi
Orodha B
SEHEMU B (ALAMA 54)
(a)Unaelewa nini dhana ya misimu
(b) Onesha vyanzo viwili vya Msimu
(c) Misimu huweza kuundwa kwa njia tofauti tofauti
Demu
Kumzimikia
Disco
Ferouz ni twiga
Mataputapu
Batuli alitaka kuhifadhi methali na vitendawili kwa njia ya Kichwa tu kwa ajili ya kizazi kijacho. Lakini Kibutu alimkataza asifanye hivyo badala yake atumie njia nyingine
Toa hoja nne (4) kama sababu ya katazo hilo
Taja njia tano (5) sahihi ambazo unahisi kibuyu angemshawishi batuli atumie.
Eleza kinagaubaga tofauti zilizopo kati ya lugha ya mazungumzo na lugha ya maandishi kwa kuzingatia vipengele vifuatavyo.
Uwasilishaji
Uhifadhi
Manadiliko
Lugha ina tabia ya kujiongeza msamiati wake kwa njia kadha wa kadha; kwa kuthibitisha dai hilo, tambulisha njia zilizotumika kuunda maneno yafuatayo.
Kuku
Mpangaji
Kifaurongo
TATAKI
Fedha
Msikwao
Kitivo
Pilipili
ix. Imla, mali, mila, lami
Maendeleo ya Sayansi na Teknologia ni ndumi la kuwili kwa fasihi simulizi. Kwa hoja sita thibitisha ukweli wa kauli hii kwa kutoa hoja mbili.
8. Soma kifungu habari kifuatacho kisha jibu maswali yanayofuata:
"Ndugu wazazi, kumbe safari yenu inahusu harusi ya Maria ?".Mkuu wa shule aliwauliza wazazi."Ndiyo," wazazi walijibu kwa Pamoja bila aibu."inategemewa kufugwa lini ."Mkuu aliendelea kuhoji. Harusi hii ilikuwa ifanyike wakati Maria anapofika kidato cha nne, Lakini Maria huyu ametufanyia uhuni na vituko visivyoelezeka. Nasi sasa tunachukiwa kijiji kizima na kudharauliwa na kila mtu.Hii imetuudhi sana, tumetungiwa nyimbo na kufanyiwa kila shutuma. Hatuna raha ;hivyo tumeonelea bora tuje kukuomba umfukuze shule ili kiburi kimwishie .Nasi tupo tayari kukulipa kiasi chochote cha fedha ukitimiza haja yetu hii,"Mzee Abdallah alieleza." Muda wote mkuu wa shule alikuwa akimtazama Mzee kwa chati sana .Kisha akauliza swali la kuchochea zaidi: Maria ana kiburi kumbe?"
Mama Maria hakutaka hilo limpite ,hima hima akatoa maelezo yake ."Mama wewe ,Maria usimuone hivi. Maria mwanangu hataki kufuata utamaduni wetu wa kuolewa. Maria ati achague mchumba mwenyewe, ati mahari haiyoni kama ni kitu cha msingi. Kiburi hicho kinatokana na elimu mliyompa.
Mtoto sasa ameharibika .Anafanya apendavyo elimu gani isiyojali adabu.wala utii?" Mama Maria alimaliza huku jasho na machozi yanamtoka".
Hapa mkuu wa shule aliona kwanza awaelimishe kabla hajawatolea kauli ya mwisho.Alikwishatambua kwamba wazazi wa Maria walikuwa wameachwa nyuma na wakati .Kila upya wa mawazo waliuita kiburi.
Maswali
(i)Bainisha dhima nne (04) zilizotokana na habari uliyosoma.
Fupisha habari hiyo kwa maneno yasiyopungua 70 na kuzidi 80.
SEHEMU C: (ALAMA 30)
Jibu maswali mawili katika sehemu hii swali la 11 ni lazima
ORODHA YA VITABU.
USHAIRI.
Wasakatonge - M.S. Khatibu (DUP).
Malenga wapya -TAKILUKI (DUP)
Mashairi ya Chekacheka - T.A.Mvungi(EP&D.LTD)
RIWAYA.
Takadini -Ben J.Hanson (MBS)
Watoto wa Mama N'tilie - E.Mbogo(HP)
Joka la Mdimu - A.J.SaiTari (HP)
TAMTHILIYA
Orodha - Steve Reynolds(MA)
Ngoswe Penzi Kitovu Cha uzembe - E. Semzaba (ESC)
Kilio chetu - Medical Aid Foundation (TPH)
9.Fasihi ya Kiswahili imemuweka mwanamke katika hadhi tofauti tofauti. Thibitisha Usemi huu kwa kutumia hoja tatu kwa kila riwaya
10.Lugha ni mhimili katika kazi yoyote ya fasihi. Watunzi hutumia lugha kiufundi ili kufikisha ujumbe kwa jamii husika. Kwa kutumia jazanda au taswira tatu kutoka katika diwani mbili ulizosoma na uonyeshe namna zinavyofikisha ujumbe kwa jamii.
11. “Ukiona mtu mzima analia ujue kuna jambo au mambo hayapo sawa. Kauli hii inaweza kuwiana na waandishi wa riwaya Juu ya jamii inavyowazunguka, kwa kutoa hoja tatu kutoka kila riwaya katika riwaya mbili ulizosoma, jadili kwa nini wasanii hao hulia
The End|Get a Copy